TAFADHALI SOMA MKATABA HUU KWA UMAKINI:-
MKATABA WA KUJIUNGA NA CHUO
UTANGULIZI KUHUSU MADRASATU TANZIIHI-LLAHI ANIL - MAKAAN
TAWI KATIKA MATAWI YA JAMAATIL-KHAIR
Madrasatu jamaatil-khair ni chuo ambacho kipo Mombasa, Mkoa wa mjini Magharibi
Zanzibar, chuo hiki hakisimamiwi na chama chochote wala mfadhili maalum.
Madhehebu rasmi yanayosomeshwa katika chuo hiki ni ya Imamu Shaafii pamoja na
kuyaheshimu madhehebu mengine yanayotambulika, na ni chuo kinachoendeshwa kwa mfumo
wa Sunni (Ahlussunna wal-jamaa) kwa mapito ya Imamu Abul-hasan al-ash-ariy.
Kwa msaada wa Allaah na tawfiq yake inshaallaah chuo kitatoa taaluma za kujifunza
kusoma Qur-an tukufu, Hadithi, pamoja na kuendesha darsa za elimu za Tawhid, Fiqhi,
Sira, Nahau, Swarfa, Tarbia Tafsiri ya Qur-an na kila taaluma itakayoonekana na
uongozi wa chuo itakayo wasaidia wanafunzi.
Chuo kina malengo ya kusomesha viwango vifuatavyo:
- kiwango cha maandalizi
- kiwango cha msingi (ibtidayya)
- kiwango cha wastani (al-idadi)
- kiwango cha sekondary (thanawiy)
Yanayo mlazimu kuyazingatia na kuyakubali mzazi/walii kabla ya kijana wake kujiunga
na chuo.
- Mtoto aneombewa kujiunga na chuo awe na umri usipungue miaka mitatu (3)
- Mzee akumbuke na kutekeleza wajibu wake kwa mtoto wake kwamujibu wa mafunzo ya
Uislamu.
- Mzee awe tayari kuhimiza mahudhurio ya kijana wake kila siku ya chuo, na pindi
mwanafunzi atatokewa na dharura yeyote ile akawa hakuhudhuria chuoni basi mzee
atawajibika kufika chuoni au kuwasiliana na uongozi wa chuo kwa ajili ya kutoa
taarifa.
- Mtoto ni lazima anunuliwe vifaa vyote vya masomo vitakavyohitajika kama vile
Juzuu, Msahafu, vitabu, madaftari, kalamu nk.
- Mzee/walii yuko huru kutoa maoni yake juu ya kijana wake au utaratibu wa chuo
kwa wanaohusika kwa madhumuni ya maendeleo ya chuo.
- Mzee/walii anatakiwa kufuata utaratibu wa kinidhamu pindi ikiwa limetokezea
tatizo kwa mtoto wake.
- Mwanafunzi anatakiwa kutii amri ya mwalimu pamoja na viongozi waliopangwa na
uongozi wa chuo.
- Mzazi/ walii/mwanafunzi atawajibika kuitikia wito mara tu atakapopewa taarifa.
- Mzazi ni lazima atoe taarifa mapema ya matatizo ya maradhi ya mwanafunzi kama
ilivyo katika kipengele cha fomu ya usaili kipengele no; 16, 17, 18.
- Mzazi/walii ni lazima azingatie usafi wa mwili na nguo za mtoto wake.
- Mzazi/walii atalazimika kumruhusu mtoto wake kuhudhuria masomo ya ziada wakati
wa usiku pindi uongozi wa chuo utakapomtaka mtoto huyo kufanya hivyo.
- Mzazi/walii atawaibika kulipa ada ya usajili wa mwanafunzi chuoni ambayo ni tsh
7000/= kwa kila mwanafunzi mpya.
- Mzazi/walii atawajibika kulipa ada ya tsh 3000/= kwa kila mwezzi, ambazo
atazilipa kidogokidogo kwa kila wiki au pamoja kwa kila mwezi au kwa mwaka mzima
kama akitaka kufanya hivyo.
- Mzazi/walii haruhusiwi kumuhamisha mtoto bila ya sanbabu ya msingi, na pindi
akifanya hivyo atawajibika kulipa fidiya atakayodaiwa na uongozi wa chuo.
- Mwanafunzi atakikanwa kukamilisha usajili ndani ya wiki mbili [2] baada ya
kuanza kuhudhuria chuoni.
- Mwanafunzi atalazimika kushonewa sare mara tu atakapojiunga na chuo na kuzivaa
kila ajapo chuoni, ikishindikana kutokana na uwezo duni wa mzazi au sababu
nyengine muwafaka chuo kitatoa muda wa miezi mitatu tu ili kupatikana sare hizo.
- Sare ya mwanafunzi atakayoivaa inatakikanwa imuwezeshe kutekeleza ibada ya sala
katika wakati wa sala na wakati wowote atakapotakikanwa kuswali.
- N.B: Mwanafunzi anatakikanwa kuvaa sare inayoendana na sheria, murua na akhlaqi
za kiislamu, kwa upande wa wanawake ni lazima sare yake ya shungi isipunguwe
kunako vidole vyake vya mikono na isidhihirishe chochote katika uso isipokuwa
ambacho sheria ya Uislamu imeruhusu, na atalazimika kuvaa soksi na ziada ya
stara nyengine pindi uongozi utakapomtaka kufanya hivyo.
- Kwa upande wa mwanamme atalazimika kuvaa kanzu nyeupe ambayo itakua inafunga juu
kwa kifungo au zipu.
- Mapambo ambayo hayanasibiani na mwanafunzi hayaruhusiwi katika mwili na kivazi.
- Mirtindo yote isiyooendana na akhlaq za kiisllam hairuhusiwi
- Mwanafunzi hatoruhusiwa kuja na chombo chochote cha electronic kama vile simu,
computer na mfano wa hivyo, ispokua atakapotakiwa na uongozi kufanya hivyo.
VIPINDI VYA MAPUMZIKO
Chuo kitakua na mapumziko kama ifuatavyo:-
- Siku ya Ijumaa na jioni ya siku ya Jumapili katika kila wiki.
- Mwezi wa nane [8] hijriya (Shaabani) kuanzia mwezi 25 hadi mwezi mosi Ramadhani.
- Mwezi wa tisa [9] hijriya (ramadhani) kuanzia mwezi 25 hadi mwezi kumi [10]
mfunguo mosi (Shawwaal)
- Mwezi wa kumi na mbili [12] mfunguo tatu (dhulhijja) kuanzia mwezi saba [7]
mpaka siku itakayoainishwa na uongozi
- Mwezi wa 12 (disember) kwa kipindi kitakachoainishwa na uongozi.
- Chuo kinaweza kua na mapumziko wakati wowote patakapotokezea sababu muafaka kama
vilke maafa, magonjwa maambukizi n.k kwa mujibu wa tamko la serikali.
وباهلل التوفيق
AHADI ZA MWANAFUNZI
Mimi………………………..……………………………………naahidi kwamba nitakua mtiifu na kutekeleza masharti
yote ya chuo, kwani nimeyakubali yote, na endapo nitakwenda kinyume au kuvunja
sheria na ahadi hii basi nipotayari kuadhibiwa, aidha nathibitisha kwamba maelezo
yote niliyoyatoa ni kweli, nikielewa kwamba kutoa taarifa za uongo kunaweza
kusababisha kunyimwa au kunyang’anywa nafasi nilioiomba.
SAHIHI YA MWANAFUNZI
…………………………….…
AHADI YA MDHAMINI
Mimi…………………………………………………………..naahidi kwamba nikotayari kudhamini mahitaji yote ya
mwanafunzi alietajwa hapo juu na kushughulikia kila linalomuhusu.
SAHIHI YA MDHAMINI
………………………………